Social Icons

Wednesday 24 February 2016

WATU 300 KUPATA HUDUMA YA UPASUAJI WA MACHO KATIKA HOSPITAL MPYA ILIYOPO CHUO KIKUU CHA DODOMA YA BENJAMIN MKAPA

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje

 Madaktari bingwa kutoka Marekani wakishirikiana na madaktari wa hapa nchini wakitoa huduma za upasuaji katika Hospital Mpya ya Benjamin Mkapa iliyopo  Chuo Kikuu cha Dodoma ya Benjamin Mkapa
 Madaktari bingwa kutoka Marekani wakishirikiana na madaktari wa hapa nchini wakitoa huduma za upasuaji katika Hospital Mpya ya Benjamin Mkapa iliyopo  Chuo Kikuu cha Dodoma ya Benjamin Mkapa

Hospital Mpya iliyopo  Chuo Kikuu cha Dodoma ya Benjamin Mkapa kwa kushirikiana na wataalamu kutoka vyuo vya UTAH (Moran aye Centre) na Chuo cha Weil Cornell Medicine vyote vya nchini Marekani wanatoa huduma za uchunguzi na matibabu ya macho. 

Vifaa vya Kisasa kabisa na madaktari bingwa hawa watakuwepo kuanzia tarehe 22 hadi 25 mwezi huu wa pili 2016.Huduma hizi zinatolewa bure kabisa. Hii ni kutoka na Mahusiano yaliyopo kati ya Chuo Kikuu cha Dodoma na vyuo hivi. 
Watu 300 wanatarajiwa kupata  huduma ya upasuaji kwa kipindi hiki. Katika Mahojiano na Dr. Jeff kutoka Chuo Kikuu cha UTAH (Moran aye Care alisema kuwa wanafanya huduma hizi pia nchi nyingi lakini kwa Dodoma tatizo ni kubwa zaidi. Alieleza kuwa mpango wao kwa sasa ni kuja Dodoma mara mbili kwa mwaka. 
Pia wanasaidia sana katika kuwafundisha madaktari wetu wa kitanzania na hadi sasa Dr. Frank ambaye ni mwalimu katika Chuo cha afya cha Chuo Kikuu cha Dodoma amefaidika na mafunzo hayo na tayari anafundisha madaktari wengine. 
 Madaktari bingwa kutoka Marekani wakishirikiana na madaktari wa hapa nchini wakitoa huduma za upasuaji katika Hospital Mpya ya Benjamin Mkapa iliyopo  Chuo Kikuu cha Dodoma ya Benjamin Mkapa
Madaktari bingwa kutoka Marekani wakishirikiana na madaktari wa hapa nchini wakitoa huduma za upasuaji katika Hospital Mpya ya Benjamin Mkapa iliyopo  Chuo Kikuu cha Dodoma ya Benjamin Mkapa.

No comments: