Social Icons

Monday 27 March 2017

#HABARI: RAIS MAGUFULI ALIAGIZA JESHI LA POLISI KUMWACHIA HURU MWANAMUZIKI NEY WA MITEGO.

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo au Habari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejephotography Twitter @Fredynjeje

 
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison George Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari Mjini Dodoma (hawapo Pichani) kuhusu agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kuachiwa huru kwa msanii wa Muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki (Ney wa Mitego) Kulia ni Naibu Waziri wake Mhe. Anastazia Wambura.


Amshauri aboreshe wimbo wake zaidi.
Amesema ni haki yake ya kujieleza.
 
Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ameliagiza Jeshi la Polisi kumwachia huru msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego kutokana na wimbo wake Wapo unaosadikiwa kukiuka madili.


Akitoa kauli hiyo kwa niaba ya Rais Magufuli, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison George Mwakyembe amesema kuwa Msanii huyo ametumia haki yake ya kikatiba ya kujieleza na ni Haki ya kila Mtanzania kujieleza kwa namna moja au nyingine pasipo kuvunja katiba ya Nchi.
 
Waziri Mwakyembe amesema Mwanamuziki huyo ni Mmoja kati ya wanamuzi wanaopendwa sana na Mhe Rais kutokana na kazi zake za muziki zinazoelimisha na kueleza changamoto mbalimbali zinakumba taifa letu.
 
“Mhe. Rais anaupenda wimbo wa msanii huyu na ameshauri auboreshe zaidi asipunguze chochote ila aongezee tu tabia nyingine ambazo hajazitaja katika wimbo wake” alisisitiza Dkt Mwakyembe.
 
Aidha Mhe. Waziri ameeleza kuwa Mhe Rais ametoa ushauri kwa msanii huyo kuboreshe wimbo huo zaidi kwani mengi aliyoyaongelea katika wimbo wake yanatokea katika jamii na kutolea mfano kama akiboresha na kuelezea zaidi kuhusu wakwepa kodi,wauzaji, wasambazaji na watumiaji madawa ya kulevya,na watanzania wasipoenda kufanya kazi kwani makundi haya yote yapo katika jamii.

No comments: